Monday, August 20, 2012

Radio Safina Facebook Page....


Bwana yesu asifiwee...
Ndugu Wana wa Mungu tunapenda kuwajulisha ya kuwa Radio Safina imetengeneza
Facebook Page ili tuzidi kueneza neno la Mungu kila kona kwa njia ya Mtandao.
Hivyo basi Wana wa Mungu tembeleeni Page yetu na Kuipenda(Like) ili uweze kutapa
mafundisho mengine kupita Ukurasa wetu Wa Facebook.

Maelekezo ya kuufikia Ukurasa wetu.      
                                                               Address:  http://www.facebook.com/RadioSafina

Yatubidi kutubu kabla mauti ayajatukuta...


Mwana wa Mungu yatubidi Kutubu kila wakati
 kwasababu hatujui Siku wala Saa.

Saturday, August 18, 2012

MAOMBI KWA AJILI YA KUPATA MWENZI (MUME/MKE)..



Maandiko: Mithali 8:22, Mithali 10:24, Zaburi 37:5
VIPENGELE VYA MAOMBI
  • Katika jina la Yesu (x3)
  • Baba wa mbinguni, ninatambua rehema na uaminifu wako maishani mwangu, utukuzwe katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Yeremia 29:11 kuwa "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya imani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho" Hivyo basi ninaomba mapenzi yako yatimizwe maishani mwangu, katika jina la Yesu.
  • Bwana, ninakuomba ninakuomba uniongeze/ uniwezeshe kukutana na atakayekuwa mwenzi wangu, katika jina la Yesu (Mwambie Mungu yale jinsi unavyotamani mwenzi wako awe). Baba nakusihi huyatende haya katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Mithali 10:24b kuwa “Na wenye haki watapata matakwa yao”, katika jina la Yesu (x2).
  • Bwana, ninajitoa kwako ili mapenzi yako yatimie. Niwezeshe kukusikia na kukutii, katika jina la Yesu.
  • Ninawakataa  wote ambao ni mawakala wa Shetani, katika jina la Yesu (x3)
  • Ninakataa  kila mpango ulioandikwa na mwovu na mawakala wake ili kunipa mwenzi asiyestahili, katika jina la Yesu.
  • Ninakuja  kinyume na roho ya tamaa ya mwili maishani mwangu, katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Mithali 18:22 kuwa “Apataye Mume (Mke) apata kitu chake; Naye ajipatia kibali kwa BWANA” Hivyo ninaomba unipatie mwenzi sawasawa na mapenzi yako, katika jina la Yesu. 
  • Asante Bwana kwa kuwa umeyasikia na kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu .

AMINA.