Wednesday, April 25, 2012

Kesho tarehe 26/4 ndo siku maalum yakung'oa Visiki.


Enyi Wana wa Mungu mnaozidi kutafakari na kutubu juu ya visiki vilivyoshikilia Malango yenu ya Ndoa, Malango ya Uchumi, Malango ya Kukosa kazi, Malango ya Kutokuolewa au kuoa n.k..  pasipo kusahau kuandaa Sadaka ya kumpendeza Mungu siku hiyo.
tunawakumbusha ya kuwa mtafakari vyema kila eneo la malango yenu yote yaliyo shikiliwa na Kisiki na kuyaandika kwenye daftari ili siku ya Al-amisi tuweze kung'oa hivyo visiki vyote vilivyoshikilia Malango yako ya maisha katika nyanja zote. Bila kusahau kuja na ule udongo tuliowaambia na kwa wale wote wanaofanya migodini na nyie mje na udongo au jiwe la kwenye mgodi ili tuweze kuomba kwa ajili ya kung'oa visiki katika maisha yetu.
Na kwa wale wote mtakaoshindwa kufika kwenye ukumbi wa Radio safina, msikose kuambatana nasi kwa njia ya Radio na Mtandao wetu  huu unaorusha matangazo ya Radio moja kwa moja.

Sio siku ya kukosa kwasababu Mungu anenda kutenda maajabu siku hiyo!

Sunday, April 22, 2012

Bwana Yesu Asifiweeee....!

Ndugu Wana wa Mungu tujitaidi kuwajuza ndugu na jamaa wanaomcha Bwana Yesu ili waweze kuitembelea hii Blog, tuwafahamishe kwa ku'share kupitia hiyo mitandao ya kijamii kwa kubofya hizo Like, Share, Send, Google + na Tweet, vile vile jiungeni ili muweze kuwa wanajumuiya kwa kubofya Join this site n.k.....

Radio Safina ipo kwa ajiri yenu Wana wa Mungu.

Mungu ni Mwema kwa kila jambo,

Monday, April 16, 2012

Je unajua yakuwa Madhabau inavyofunga nafsi zetu..!

Ndugu mpendwa mwana wa Mungu Jumanne hii ya Terehe 17/April sio siku ya kukosa kwenye ukumbi wa Radio Safina kwasababu ni siku ya kwenda kuvunja Madhabau zote zilizo shikiria Nafsi zetu ivyo basi njooni  nyote ili tuweze kukomboa Nafsi ....

Sunday, April 8, 2012

“Kheli ya Pasaka wana wa Mungu” Bwana Yesu katukomboa kwa msalaba wake mtakatifu!


Ndugu wana wa Mungu mnakaribishwa nyote kuja kutoa shukrani zako kwa Yesu ndani ya Madhabau ya Radio Safina kwa kuwa kutukomboa  kwa msalaba wake mtakatifu, hivyo basi mnakaribishwa nyote siku ya Jumanne, ili kuzidi kumuabudu Yesu kwa kuwa yeye ndo Bwana wa Mabwana.
Usisahau kuja na kitambaa chako cheupe kwa ajili ya kumtukuza Yesu…….

Friday, April 6, 2012

Mtumishi wa Mungu Mr Jovin Abel.

Mtumishi wa Mungu Mr Jovin Abel ndani ya Radio Safina
anayeendesha vipindi vya Njia ya Vijana, Tutembelee Biblia,
na Safari ya msafiri.

Visiki vyazidi kung'olewa ndani ya Radio Safina!

Shughuli ya kungoa Visiki ndani ya Radio Safina yazidi kuendelea kila siku ya Alhamisi ndani ya Madhabau ya Radio Safina, ndugu wana wa Mungu ebu jongeeni ili tuweze kushugulikia Visiki vinavyozitesa nafsi zetu na kusababisha matatizo ndani ya maisha yetu.......!

Njooni nyote tungoeni visiki......