Saturday, February 23, 2013

Viwanja vya Sheik Amri Abeid leo vya fulika..

Bwana Yesu Asifiwe.

Kwa wale wote waliofatilia kipindi chetu siku ya leo ndani ya Viwanja vya Sheik Amri Abeid mjini Arusha leo siku ya tarehe 23/02/2013. Kwa maombi ya Toba kila mtu amechota baraka za kutosha, na tunaimani ya kuwa wale wote waliotufatilia kwa njia ya Radio kupitia Mtandao tunaimani nanyi Mmebarikiwa na Toba yenu Mungu kaipokea kuweni na Imani nazidi kufatilia vipindi vyetu vinvyoendelea.

Amina.

Tuesday, February 12, 2013

UNAPOOTA UNAONA DAMU AU JENEZA.


VIPENGERE VYA MAOMBI:

  1. Damu ya Yesu (x7)
  2. Baba wa milele, ninakuja kinyume na nguvu zote za giza zisababishazo uharibifu wa mimba zangu, katika jina la Yesu.
  3. Ninatangaza kufuta mipango yote ya mwovu aliyekuwa ameipanga kusababisha ajali au kifo, kwangu na familia yangu, katika jina la Yesu.
  4. Ewe pepo wa mauti ninakufunga na kukutupa mbali na maisha yangu, katika jina la Yesu (x2)
  5. Ninampiga Upofu Shetani na mawakala wake wote walio kinyume nami, katika jina la Yesu.
  6. Ninajizamisha damuni mwa Yesu (mwili, nafsi na roho) (x2)
  7. (Kwa Wanawake wajawazito) Ewe pepo usababishaye uharibifu wa mimba, ninakuamru utoke maishani mwangu na familia yangu, katika jina la Yesu(x3)
  8. Ninaangusha kila ngome ya adui iliyoko dhidi ya maisha yangu katika jina la Yesu.
  9. Asante Bwana kwa kunipa ushindi dhidi ya nguvu za giza, katika jina la Yesu.
         Amina.

ANGALIZO: Kama hali itaendelea, fanya maombi ya kufunga kwa siku 3 mfululizo.