Wednesday, June 28, 2017

Maombi ya Kupata Mwenza (Mume/Mke)

Maandiko: Mithali 8:22, Mithali 10:24, Zaburi 37:5
VIPENGELE VYA MAOMBI
 • Katika jina la Yesu (x3)
 • Baba wa mbinguni, ninatambua rehema na uaminifu wako maishani mwangu, utukuzwe katika jina la Yesu.
 • Imeandikwa katika Yeremia 29:11 kuwa "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya imani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho" Hivyo basi ninaomba mapenzi yako yatimizwe maishani mwangu, katika jina la Yesu.
 • Bwana, ninakuomba ninakuomba uniongeze/ uniwezeshe kukutana na atakayekuwa mwenzi wangu, katika jina la Yesu (Mwambie Mungu yale jinsi unavyotamani mwenzi wako awe). Baba nakusihi huyatende haya katika jina la Yesu.
 • Imeandikwa katika Mithali 10:24b kuwa “Na wenye haki watapata matakwa yao”, katika jina la Yesu (x2).
 • Bwana, ninajitoa kwako ili mapenzi yako yatimie. Niwezeshe kukusikia na kukutii, katika jina la Yesu.
 • Ninawakataa  wote ambao ni mawakala wa Shetani, katika jina la Yesu (x3)
 • Ninakataa  kila mpango ulioandikwa na mwovu na mawakala wake ili kunipa mwenzi asiyestahili, katika jina la Yesu.
 • Ninakuja  kinyume na roho ya tamaa ya mwili maishani mwangu, katika jina la Yesu.
 • Imeandikwa katika Mithali 18:22 kuwa “Apataye Mume (Mke) apata kitu chake; Naye ajipatia kibali kwa BWANA” Hivyo ninaomba unipatie mwenzi sawasawa na mapenzi yako, katika jina la Yesu. 
 • Asante Bwana kwa kuwa umeyasikia na kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu .


AMINA.