Huduma


MAOMBI NA MASOMO YALETAYO MIUJIZA:

KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA
Maandiko: ufunuo 3:8, II Korint. 2:12, Malaki 3:10-12, Malaki 1:10
VIPENGERE VYA MAOMBI
 •      Katika jina la Yesu (Mara 3) 
 •      Mwamba wangu wa kale, ninakuhabudu.  Uinuliwe katika jina la Yesu
 •      Milango yote iliyofungwa ninaiamru ifunguke, katika jina la Yesu (x2)
 •      Ninaamru radi toka juu ibomoe kila ufunguo uliotumika kuyafunga mafanikio   yangu,  katika jina la Yesu (x3)
 •     Ninaufungua mwili wangu, nafsi na roho kutoka katika kila kifungo cha Shetani  katika jina la Yesu (x3)
 •    Ninaamru udhihirisho wa Baraka kutoka MASHARIKI, MAGHARIBI, KASKAZINI na KUSINI, katika jina la Yesu. Amina
 •   Milango yote inayoingiza uchafu ninaimru ifunguke katika jina la Yesu (x3)
 •   Ninaizamisha biashara yangu, mali na familia yangu kwenye damu ya Yesu (x2)
 •  Utukuzwe Bwana kwa kuwa umeyajibu maombi yangu katika jina la Yesu.

AMINA.

2.MAOMBI DHIDI YA UCHAWI NA MASHAMBULIZI YA KICHAWI.

Vipengere vya maombi


 1. Moto wa Roho Mtakatifu(Rudia Mara 7), Damu ya Yesu(Mara 7)
 2. Baba katika jina la Yesu, ninakuja kwako nikisihi damu ya Yesu itakase nafsi yangu, roho na mwili pia.
 3. Imeandikwa katika Isaya 54:17 kuwa “Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa”. Na ninatamka sasa kuwa kila silaha ya kichawi iliyo kinyume nami haitafanikiwa katika jina la Yesu.
 4. Popote pale ambako jina langu, pesa zangu ama mali zangu zimechukuliwa katika ulimwengu wa roho, ninazidhoofisha nguvu hizo katika jina la Yesu (rudia mara 2)
 5. Imeandikwa katika Mithali 18:10 kuwa “Jina la Bwana ni ngome imara. Mwenye haki hukimbilia na kuwa salama”. Ninadai usalama wangu sasa dhidi ya kila nguvu ya adui katika jina la Yesu.
 6. Ninawafunga wachawi wote wanaoshambulia maisha yangu katika jina la Yesu.
 7. Ninawatosa adui zangu wote kwenye moto wa roho Mtakatifu. Wakakose amani mpaka apo watakapotubu.
 8. Kila mshale uliorushwa kwangu, ninauzuia kwa kutumia ngao ya Roho Mtakatifu na ninauamuru uwarudie walioutuma, katika jina la Yesu.(Rudia mara 3)
 9. Ninanyunyizia damu ya Yesu juu ya kila kioo watakachotumia kutaka kuibua taswira yangu na ninaamuru radi kutoka mbinguni ikavunjevunje, katika jina la Yesu. (Rudia mara 3)
 10. Kupitia damu ya Yesu, ninafuta athari zote zitokanazo na vitu vyote vya kipepo watakavyonitupia ili nivikanyage, katika jina la Yesu.
 11. Hata kama wataniwekea sumu kwenye chakula changu ama kinywaji, ninaibatilisha sumu hiyo kwa kutumia damu ya Yesu. (Rudia mara 3)
 12. Ninaizamisha nafsi yangu, mwili na roho katika damu ya Yesu. (mara 3)
 13. Ninaharibu kila nguvu ya kichawi iliyoko dhidi ya maisha yangu, katika jina la Yesu. (Rudia mara 3)
 14. Popote na kwa yeyote yule ambaye anatumiwa na Shetani, awe ni baba yangu, mama, dada, kaka, shemeji au wifi ninawatamkia kutofanikiwa katika njia zoa, katika jina la Yesu.
 15. Ninaifunika familia yangu, biashara na mali zangu zote kwa damu ya Yesu. (Rudia mara 3)
 16. Baba, achilia malaika wako wanilinde mimi na vyote nilivyonavyo, katika jina la Yesu.
ANGALIZO: Kama mashambulizi yatang’ang’ania, funga kuanzia saa 12 alfajili hadi 12 jioni kwa siku 3 mfululizo huku ukiomba kila siku.