Thursday, May 29, 2014

MAOMBI WAKATI WA UJAUZITO

Maandiko: Zabuaria 127:3, Mwanzo 1:28.
VIPENGERE VYA MAOMBI
 1. Damu ya Yesu(x3); Katika jina la Yesu (x3)
 2. Baba wa mbinguni, Muumba mbingu na nchi, ninakuabudu.  Bwana, ninayakabidhi kwako maisha yangu na ya  mtoto aliyeko tumboni mwangu ili uyatawale, katika jina la Yesu.
 3. Maendeleo yote ya mtoto huyu ninayaacha mikononi mwako.
 4. Bwana, tupatie fedha mimi na mume wangu ili tuweze kumlea na kumtunza mtoto huyu, katika jina la Yesu.
 5. Ninaagiza moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila mkono mbaya utakaogusa tumbo hili kwa lengo la kuharibu ujauzito huu, katika jina la Yesu (x3).
 6. Ninalipiga upofu kila jicho lenye hila dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3)
 7. Ninabatilisha kila shambulizi la kipepo dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3).
 8. Popote pale ambapo kuna wachawi wanaopanga kumchukua mwanangu, ninafutilia mbali jitiada zao hizo na kuamru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze hadi pale watakapomwaachia mwanangu, katika jina la Yesu.
 9. Ninaharibu kila hali za Shetani na mawakala wake huko hospitalini, nyumbani, au popote pale, ambazo zimeandaliwa kunizuia nisijifungue salama, katika jina la Yesu (x3).
 10. Ninajizamisha damuni mwa Yesu mimi na mwanangu, katika jina la Yesu (x3).
 11. Ninatamka na kudai usalama wa maisha yangu na mwanangu aliyeko tumboni, katika jina la Yesu(x3).
 12. Ninaifunika kwa damu ya Yesu nyumba yangu pamoja na hospitali nitakayokwenda kujifungulia (itaje jina).
 13. Ninatamka kuwa manesi na madaktari wa hospitali hii (itaje jina) watafanyika vyombo vya Mungu vitakavyonisaidia nijifungue salama. Katika jina la Yesu.
 14. Asante Bwana kwa kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu.
Amina..

Thursday, March 27, 2014

Maombi siku ya tarehe 22/03/2014 Arusha.

Hivi ndivyo ilivyokuwa siku ya j'mosi ya tarehe 22/03/2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha kwa ajiri ya maombi maalum kwa wakina mama wote...Yesu anatupenda.
Amen


Monday, January 13, 2014

MAOMBI KABLA YA KUFUNGA NDOA


Maandiko: Mithali 18:22, Zaburi 37:5

 • Moto wa roho mtakatifi (x3) katika jina la Yesu (x3)
 • Mungu uishiye mahari pa juu na Baba wa milele, ninakusifu na kukuabudu.
 • Imeandikwa kuwa “Apataye mke (mume) apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA “ Hivyo basi nadai upendeleo katika yote ninayofanya, katika jina la Yesu.
 • Bwana, ninakuomba utufanyie njia mimi na mwenzi wangu, Tupatie fedha na usaidizi wa kutosha wenye kuleta mafanikio katika harusi yetu, katika jina la Yesu (x3)
 • Ninamzamisha mke (Mume) wangu mtarajiwa kwenye damu ya Yesu
 • Ninampiga upofu shetani na maajenti wake ili wasimwone, katika jina la Yesu (x2)
 • Tukinge na ajari katika njia zote tutakazoziendea, katika jina la Yesu.
 • Bwana, tjalie upendeleo wa Kiungu kwa kila tutakaemwendea, katika jina la Yesu.
 • Ninakuja kinyume na Falme na mamlaka zote zilizo kinyume na harusi yetu, katika jina la Yesu.
 • Ninavuruga kila mpango wa Yule mwovu ulioandaliwa kuharibu ndoa yetu, katika jina la Yesu.
 • Ninafunga kila pepo lililoandaliwa kupinga ndoa yetu, katika jina la Yesu.
 • Baba,  ifanye harusi yetu kuwa yenye mafanikio, pokea utukufu katika jina la Yesu.

Amina.


ANGALIZO:  Funga kwa siku 2, kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni huku ukiomba maombi haya.

Saturday, September 7, 2013

Changia Radio Safina ili izidi kuenea Ulimwengu mzima.

Enyi Wana wa Mungu, ni vyema kama tutaichangia Radio safina ili iweze kupeperusha vyema Bendela yake ya kueneza neno la mungu Nchi nzima pamoja na Ulimwengu mzima, ni mikoa michache iyayosikiliza neno la mungu moja kwa moja kupia Radio, ivyo hatuna budi kuchangia ili izidi kutanuka na kusikilizwa kila Mkoa. 

Mbarikiwe sana wale wote mnaotupata kwa njia ya Radio pamoja na Mtandao.

Amina.

Friday, July 26, 2013

VIPENGERE VYA MAOMBI YA UGONJWA USIOJULIKANA.

Maandiko:  Kumb. 1:7-15, 3Yohana 2, Isaya 10:27

VIPENGERE VYA MAOMBI:


 •     Damu ya Yesu (x7), katika jina la Yesu (x7), Moto wa Roho Mtakatifu (x3).
 •    Yehova Rafa, ninakubariki katika jina la Yesu.
 •   (Weka mikono juu ya sehemu husika) Kila kilichopandikizwa na mwovu au wakala wake, ninaamru kwa mamlaka ya jina la Yesu kiteketezwa na moto wa Roho Mtakatifu.
 •  Kila mbegu ya ugonjwa mwilini mwangu, ninakiamru ife katika jina la Yesu (x3)
 •   Chochote kinachotembeatembea mwilini mwangu ninakiamru kiondoke katika jina la Yesu (x2)
 •  Ewe pepo ulietumwa kwangu, ninakung’oa  na kukuteketeza kwa moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la Yesu.
 •  Sikia ewe ugonjwa usiyejulikana imeandikwa kuwa “Kwa kupigwa kwake mimi nimepona” Hivyo basi, ninakuamuru uachie mwili wangu (toka katika jina la Yesu) (x3).
 •  Asante Bwana kwa kuwa umenipanya, katika jina la Yesu.
       Amina.