Thursday, May 29, 2014

MAOMBI WAKATI WA UJAUZITO

Maandiko: Zabuaria 127:3, Mwanzo 1:28.
VIPENGERE VYA MAOMBI
 1. Damu ya Yesu(x3); Katika jina la Yesu (x3)
 2. Baba wa mbinguni, Muumba mbingu na nchi, ninakuabudu.  Bwana, ninayakabidhi kwako maisha yangu na ya  mtoto aliyeko tumboni mwangu ili uyatawale, katika jina la Yesu.
 3. Maendeleo yote ya mtoto huyu ninayaacha mikononi mwako.
 4. Bwana, tupatie fedha mimi na mume wangu ili tuweze kumlea na kumtunza mtoto huyu, katika jina la Yesu.
 5. Ninaagiza moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila mkono mbaya utakaogusa tumbo hili kwa lengo la kuharibu ujauzito huu, katika jina la Yesu (x3).
 6. Ninalipiga upofu kila jicho lenye hila dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3)
 7. Ninabatilisha kila shambulizi la kipepo dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3).
 8. Popote pale ambapo kuna wachawi wanaopanga kumchukua mwanangu, ninafutilia mbali jitiada zao hizo na kuamru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze hadi pale watakapomwaachia mwanangu, katika jina la Yesu.
 9. Ninaharibu kila hali za Shetani na mawakala wake huko hospitalini, nyumbani, au popote pale, ambazo zimeandaliwa kunizuia nisijifungue salama, katika jina la Yesu (x3).
 10. Ninajizamisha damuni mwa Yesu mimi na mwanangu, katika jina la Yesu (x3).
 11. Ninatamka na kudai usalama wa maisha yangu na mwanangu aliyeko tumboni, katika jina la Yesu(x3).
 12. Ninaifunika kwa damu ya Yesu nyumba yangu pamoja na hospitali nitakayokwenda kujifungulia (itaje jina).
 13. Ninatamka kuwa manesi na madaktari wa hospitali hii (itaje jina) watafanyika vyombo vya Mungu vitakavyonisaidia nijifungue salama. Katika jina la Yesu.
 14. Asante Bwana kwa kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu.
Amina..