Wednesday, February 26, 2020

MAOMBI KWA AJILI YA KUPATA MWENZI (MUME/MKE)..

Maandiko: Mithali 8:22, Mithali 10:24, Zaburi 37:5
VIPENGELE VYA MAOMBI
  • Katika jina la Yesu (x3)
  • Baba wa mbinguni, ninatambua rehema na uaminifu wako maishani mwangu, utukuzwe katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Yeremia 29:11 kuwa "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya imani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho" Hivyo basi ninaomba mapenzi yako yatimizwe maishani mwangu, katika jina la Yesu.
  • Bwana, ninakuomba ninakuomba uniongeze/ uniwezeshe kukutana na atakayekuwa mwenzi wangu, katika jina la Yesu (Mwambie Mungu yale jinsi unavyotamani mwenzi wako awe). Baba nakusihi huyatende haya katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Mithali 10:24b kuwa “Na wenye haki watapata matakwa yao”, katika jina la Yesu (x2).
  • Bwana, ninajitoa kwako ili mapenzi yako yatimie. Niwezeshe kukusikia na kukutii, katika jina la Yesu.
  • Ninawakataa  wote ambao ni mawakala wa Shetani, katika jina la Yesu (x3)
  • Ninakataa  kila mpango ulioandikwa na mwovu na mawakala wake ili kunipa mwenzi asiyestahili, katika jina la Yesu.
  • Ninakuja  kinyume na roho ya tamaa ya mwili maishani mwangu, katika jina la Yesu.
  • Imeandikwa katika Mithali 18:22 kuwa “Apataye Mume (Mke) apata kitu chake; Naye ajipatia kibali kwa BWANA” Hivyo ninaomba unipatie mwenzi sawasawa na mapenzi yako, katika jina la Yesu. 
  • Asante Bwana kwa kuwa umeyasikia na kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu .


AMINA.

Wednesday, June 28, 2017

Nami nitamkiri

“Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

Thursday, May 29, 2014

MAOMBI WAKATI WA UJAUZITO

Maandiko: Zabuaria 127:3, Mwanzo 1:28.
VIPENGERE VYA MAOMBI
  1. Damu ya Yesu(x3); Katika jina la Yesu (x3)
  2. Baba wa mbinguni, Muumba mbingu na nchi, ninakuabudu.  Bwana, ninayakabidhi kwako maisha yangu na ya  mtoto aliyeko tumboni mwangu ili uyatawale, katika jina la Yesu.
  3. Maendeleo yote ya mtoto huyu ninayaacha mikononi mwako.
  4. Bwana, tupatie fedha mimi na mume wangu ili tuweze kumlea na kumtunza mtoto huyu, katika jina la Yesu.
  5. Ninaagiza moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila mkono mbaya utakaogusa tumbo hili kwa lengo la kuharibu ujauzito huu, katika jina la Yesu (x3).
  6. Ninalipiga upofu kila jicho lenye hila dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3)
  7. Ninabatilisha kila shambulizi la kipepo dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x3).
  8. Popote pale ambapo kuna wachawi wanaopanga kumchukua mwanangu, ninafutilia mbali jitiada zao hizo na kuamru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze hadi pale watakapomwaachia mwanangu, katika jina la Yesu.
  9. Ninaharibu kila hali za Shetani na mawakala wake huko hospitalini, nyumbani, au popote pale, ambazo zimeandaliwa kunizuia nisijifungue salama, katika jina la Yesu (x3).
  10. Ninajizamisha damuni mwa Yesu mimi na mwanangu, katika jina la Yesu (x3).
  11. Ninatamka na kudai usalama wa maisha yangu na mwanangu aliyeko tumboni, katika jina la Yesu(x3).
  12. Ninaifunika kwa damu ya Yesu nyumba yangu pamoja na hospitali nitakayokwenda kujifungulia (itaje jina).
  13. Ninatamka kuwa manesi na madaktari wa hospitali hii (itaje jina) watafanyika vyombo vya Mungu vitakavyonisaidia nijifungue salama. Katika jina la Yesu.
  14. Asante Bwana kwa kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu.
Amina..

Thursday, March 27, 2014

Maombi siku ya tarehe 22/03/2014 Arusha.

Hivi ndivyo ilivyokuwa siku ya j'mosi ya tarehe 22/03/2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha kwa ajiri ya maombi maalum kwa wakina mama wote...Yesu anatupenda.
Amen


Monday, January 13, 2014

MAOMBI KABLA YA KUFUNGA NDOA


Maandiko: Mithali 18:22, Zaburi 37:5

  • Moto wa roho mtakatifi (x3) katika jina la Yesu (x3)
  • Mungu uishiye mahari pa juu na Baba wa milele, ninakusifu na kukuabudu.
  • Imeandikwa kuwa “Apataye mke (mume) apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA “ Hivyo basi nadai upendeleo katika yote ninayofanya, katika jina la Yesu.
  • Bwana, ninakuomba utufanyie njia mimi na mwenzi wangu, Tupatie fedha na usaidizi wa kutosha wenye kuleta mafanikio katika harusi yetu, katika jina la Yesu (x3)
  • Ninamzamisha mke (Mume) wangu mtarajiwa kwenye damu ya Yesu
  • Ninampiga upofu shetani na maajenti wake ili wasimwone, katika jina la Yesu (x2)
  • Tukinge na ajari katika njia zote tutakazoziendea, katika jina la Yesu.
  • Bwana, tjalie upendeleo wa Kiungu kwa kila tutakaemwendea, katika jina la Yesu.
  • Ninakuja kinyume na Falme na mamlaka zote zilizo kinyume na harusi yetu, katika jina la Yesu.
  • Ninavuruga kila mpango wa Yule mwovu ulioandaliwa kuharibu ndoa yetu, katika jina la Yesu.
  • Ninafunga kila pepo lililoandaliwa kupinga ndoa yetu, katika jina la Yesu.
  • Baba,  ifanye harusi yetu kuwa yenye mafanikio, pokea utukufu katika jina la Yesu.

Amina.


ANGALIZO:  Funga kwa siku 2, kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni huku ukiomba maombi haya.