Wednesday, April 25, 2012

Kesho tarehe 26/4 ndo siku maalum yakung'oa Visiki.


Enyi Wana wa Mungu mnaozidi kutafakari na kutubu juu ya visiki vilivyoshikilia Malango yenu ya Ndoa, Malango ya Uchumi, Malango ya Kukosa kazi, Malango ya Kutokuolewa au kuoa n.k..  pasipo kusahau kuandaa Sadaka ya kumpendeza Mungu siku hiyo.
tunawakumbusha ya kuwa mtafakari vyema kila eneo la malango yenu yote yaliyo shikiliwa na Kisiki na kuyaandika kwenye daftari ili siku ya Al-amisi tuweze kung'oa hivyo visiki vyote vilivyoshikilia Malango yako ya maisha katika nyanja zote. Bila kusahau kuja na ule udongo tuliowaambia na kwa wale wote wanaofanya migodini na nyie mje na udongo au jiwe la kwenye mgodi ili tuweze kuomba kwa ajili ya kung'oa visiki katika maisha yetu.
Na kwa wale wote mtakaoshindwa kufika kwenye ukumbi wa Radio safina, msikose kuambatana nasi kwa njia ya Radio na Mtandao wetu  huu unaorusha matangazo ya Radio moja kwa moja.

Sio siku ya kukosa kwasababu Mungu anenda kutenda maajabu siku hiyo!